Naibu Waziri Mambo ya ndani ya nchi Eng. Hamad Massauni ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kumtafuta Mbunge wa Iringa mjini Pater Msigwa ili awasaidie kupata taarifa za kupatikana kwa mwanachama wa CHADEMA maarufu kama Mdude Chadema anayedaiwa kupotea (kutekwa) katika siku za hivi karibuni katika mkoa wa Songwe, Waziri Massauni ameoa maagizo hayo baada ya Msigwa kulieleza Bunge kuwa Mdude Chadema hajapotea bali ametekwa.
“Mbunge Msigwa amesema kuwa Mdude Chadema ametekwa na Polisi wamekataa kufungua jarada kitu ambacho sio sahihi, ukweli wa mtu huyu hakuonekana na ukisema ametekwa inamaana wewe hunajua na bila shaka Msigwa ana taarifa hizo na nilielekeze Jeshi la Polisi limtafute Msigwa ili aisaidie Polisi”- Eng. Hamad Massauni
Taarifa rasmi ya CHADEMA juu ya Mdude Nyagali kuchukuliwa na wasiojulikana