Top Stories

UTEKAJI MWANZA: Mama asimulia kila kitu Mtoto kutekwa, Mtekaji ataka Mil 3 M-Pesa

on

Mwishoni mwa August 2017 huko Mwanza kulikuwa na mtoto ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la Kwanza mwenye umri wa miaka 8 ambaye alitekwa na mtu asiyefahamika kisha Mama yake akapigiwa simu na Mtekaji huyo akitaka amtumie Tsh Milioni 3 ili arudishiwe mtoto wake.

Ayo TV na millardayo.com zimemtafuta mama huyo ambaye anasimulia mkasa mzima kuanzia mwanzo wa tukio hadi pale alipopata ujumbe kutoka kwa mtekaji uliomtaka atume fedha Tsh Milioni 3 ili amkomboe mtoto wake.

>>>”Kama mama iliniumiza sana. Siku mbili mtoto hajapatikana nyumbani, sikula wala kulala…alinitumia text majira ya saa sita siku hiyo hiyo baada ya kufanya juhudi za kumtafuta tumemkosa, tumeenda kituoni tukaambiwa baada ya saa 24 tukarudi nyumbani.

“Tumekaa mida ya saa sita ndiyo akatuma hiyo meseji kwamba ‘mtoto wako ninaye, tuma hela Milioni 3 tukupe mtoto wako’.” – Mama wa Mtoto.

HUZUNI HARUSINI!!! Mabwana harusi waugua baada ya kula chakula chenye sumu

SHAMBULIZI LA CHUI: Majeruhi asimulia alivyonusurika kuuawa

Soma na hizi

Tupia Comments