Kama unakumbuka August 24 2016 jeshi la polisi nchini lilipiga marufuku mikutano na vikao vyote vya ndani kwa vyama vya siasa mpaka pale hali ya usalama itakapotengemaa.
Leo September 22 2016 taarifa imetolewa na jeshi la polisi nchini kupitia kwa Kamishna wa operesheni na mafunzo, Nsato Marijani Mssanzya amesema kuwa wamekuwa wakifuatilia hali ya usalama hasa inayohusiana na shughuli ya vyama vya siasa na sasa jeshi la polisi limejiridhisha kwamba kumekuwepo na hali ya kuridhisha kiusalama na hivyo kuona hakuna hoja ya kiusalama ya kuendelea kuzuia mikutano ya ndani.
Hivyo jeshi hilo limesema kuanzia leo September 22 2016 linaondoa katazo la mikutano ya ndani ya vyama vya siasa. Aidha jeshi la polisi limesisitiza kuwa maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa isipokuwa ile ya waheshimiwa wabunge katika majimbo yao bado imezuiliwa hadi tahthmini pana ya hali ya usalama itakapofanyika.
#MillardAyoUPDATES Taarifa kamili ya Polisi kuhusu mikutano ya vyama vya siasa na lile katazo lililotolewa. pic.twitter.com/vJ2b0ipEzy
— millardayo (@millardayo) September 22, 2016
ULIKOSA MADEREVA WALIOTEKWA CONGO KUSIMULIA YALIYOTOKEA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI