Ad

Top Stories

Polisi Marekani yapata taarifa za kijasusi kuvamiwa Bunge

on

Polisi Nchini Marekani wamesema wamepata taarifa za ujasusi za kuwepo kwa njama ya kuvamiwa tena kwa majengo ya Bunge la Marekani maarufu kama Capitol mjini Washington.

Taarifa hizo za ujasusi zinatokea takriban miezi miwili tu baada ya Wafuasi wa aliyekuwa Rais Donald Trump kuyavamia majengo ya Bunge hilo ili kujaribu kulizuia Bunge kuthibitisha ushindi wa Rais wa sasa Joe Biden.

Tishio la uvamizi huo linahusishwa na Wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia, hasa wanaotokea kwenye kundi la QAnon linalohusishwa na imani ya kishirikina na ambalo linaamini kuwa Trump atarudi tena madarakani.

Tangazo hilo linatokea katika wakati ambapo Polisi wanaolinda majengo ya Bunge wamekosolewa kwa jinsi walivyoshughulikia uvamizi wa majengo hayo January 06,2021.

MAPYA GENIUS WA HESABU APATA SHULE YA KISHUA “KURUSHWA DARASA NI KIBOKO, ANAWAZIDI DARASA LA SABA”

Soma na hizi

Tupia Comments