Top Stories

Polisi Simiyu yamnasa aliyebaka Mtoto wa miaka mitano

on

Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu, linamshikilia Mkazi wa Wilaya ya Bariadi, Ndamo Mabula (25) kwa tuhuma za kumbaka Mtoto mdogo wa miaka mitano (5) baada ya kumvizia mtoto huyo wakati wazazi wake wamekwenda shambani na kisha kutekeleza kitendo hicho cha kikatili na kwamba Jeshi hilo linatarajia kumfikisha Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa Kijana huyo.

Baada ya kijana huyo kufanya kitendo hicho alikimbia huku mtoto huyo akipiga kelele za kuomba msaada na ndipo Wananchi walipojitokeza kumsaidia na alipoulizwa aliweza kumtaja kijana huyo na hivyo Wananchi wakaanza kumtafuta na kufanikiwa kumkamata na kisha kumfikisha Polisi.

BASHUNGWA ATANGAZA MAREKEBISHO YA SHERIA YA POMBE YA KIENYEJI “KUNA SHERIA KANDAMIZI”

Soma na hizi

Tupia Comments