Top Stories

Polisi, Vyama vya Siasa kukutana September 23

on

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeweka mpango mkakati wa kuandaa vikao vya wadau kati ya wadau mbalimbali wa siasa na Jeshi la Polisi nchin kwa lengo la kuondoa changamoto zinazojitokeza baina yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi, amesema nia ya vikao hivyo ni kuweka mazingira rafiki na maelewano baina ya vyama vya Siasa.

Jaji Mtungi amesema kikao cha kwanza cha wadau kitafanyika Septemba 23 mwaka huu ambapo ofisi hiyo itakutana na Jeshi la Polisi nchini kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi juu ya malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vyama vya Siasa katika ofisi hiyo.

“Mkutano huu utaendeshwa bila ya kuepo upendeleo kwani utaendeshwa na Waziri ambaye ana mafungano ya vyama siasa ili kutia fursa kwa vyama vya siasa kuelezea chagamoto zinazowakabili na kufikia Maridhiano” Jaji Mtungi.

LIVE: ASKARI ALEMUUA HAMZA ANASIMULIA

Soma na hizi

Tupia Comments