Ad
Ad

Top Stories

Polisi wafunguka kuhusu shamra shamra za sikukuu ya PASAKA ‘hatujapiga marufuku’

on

Ni Headlines za Jeshi la Polisi ambapo leo April 2, 2021 wametoa ufafanuzi juu ya kauli waliyoitoa kuhusu shamra shamra za kusheherekea sikukuu za Pasaka.
Taarifa ya Jeshi la Polisi niliyoitoa jana (pamoja na mambo mengine) ilisema tuna imani kama kila Mwananchi atafuata Sheria na kujiepusha na vishawishi vya kufanya uhalifu, Ibada ya Pasaka itamalizika salama na hatutegemei zile Sherehe na Shamrashamra tulizozizoea kipindi cha miaka ya nyuma kuwepo katika kipindi hiki, kwa bahati mbaya taarifa hiyo ilipokewa na tafsiri tofauti kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku Sherehe za Pasaka”– David Misime-SACP, Msemaji wa Polisi

“Jeshi la Polisi halijapiga marufuku Sherehe za Pasaka na ndio maana hata jana Ibada ya Sikukuu ya Alhamisi Kuu ilifanyika Nchi nzima bila bughudha yeyote na Askari wetu waliovaa sare za Polisi na waliovaa kiraia walikuwa doria kuhakikisha amani, utulivu na usalama unakuwepo”———POLISI

“Jambo ambalo hatutegemei kuliona ni zile shamrashamra kubwa kama vile Matamasha na Makongamano ya Pasaka na kwa bahati nzuri wanaoyaandaa kila mwaka kwa utu wao wa Kitanzania, hekima na busara zao hatujasikia wakitangaza maandalizi ya Matamasha hayo”-POLISI

“Ibada za Sherehe za Pasaka kwenye Makanisa, Sherehe za Kifamilia, Hitma, Familia kuungana na kwenda kutembelea sehemu mbalimbali na kusherehekea Pasaka hakuna aliyekataza ili mradi unachofanya kinaendana na kufuata utu, busara, hekima, Sheria , kanuni na taratibu za Nchi”-POLISI

Tupia Comments