Top Stories

Mama ataka kujiua, Mtoto alieshindwa kufika Form 4 ajiua, wawili watupwa shimoni (+video)

on

Mwanamke mmoja mkazi wa Mtaa wa Nike Kata ya Goba Dare es salaam anadaiwa kuwatupa Watoto wake kwenye shimo la maji ya mvua na kisha kunywa sumu ili ajiue.

Katika tukio hilo Mtoto wake mkubwa ambaye amemaliza kidato cha nne mwaka jana amefariki ikiaminika amejinyonga au kunyongwa huku Mwanamke huyo akihisiwa pia kuhusika.

“Mumewe alifariki akabaki na Familia lakini baadaye akawa analalamika maisha yamekuwa magumu, Watoto wote watatu walirudishwa kutoka shule kwa kukosa ada, aliniambia anataka kuweka gari bondi apate pesa, hakuwa na pesa alikuwa anafuatilia mirathi” -Ahmed Abdalla, Jirani

RPC Kinondoni, Ramadhani Kingai amethibitisha kupata taarifa hizo na kusema bado wanafuatilia zaidi na watatoa taarifa.

RAIS MAGUFULI AKIMKAMUA NG’OMBE MAZIWA

Soma na hizi

Tupia Comments