Top Stories

Polisi washangazwa kumkuta hai mtu kwenye tairi la ndege

on

Polisi wa kijeshi nchini Uholanzi wameshangazwa kumkuta mtu aliyekuwa amejificha chini ya ndege kwenye eneo la tairi la mbele kuwa yuko salama.

Ndege hiyo ilisafiri kwa masaa 11 kutokea Afrika mpaka Ulaya.

Ndege hiyo ya mizigo ilitokea Afrika Kusini na kutua Kenya kwa muda mfupi kabla ya kuelekea Amsterdam, Uholanzi.

Mtu huyo ambaye uraia wake, jinsia na umri bado havijatajwa sasa yuko hospital na hali yake inaendelea vizuri.

Uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea lakini Polisi hao wamesisitiza kuwa “hii ni ngumu kuielewa, ukizingatia baridi ya sehemu alipokuwa amejificha na urefu kutoka usawa wa bahari ndege hiyo aina ya Boeing 747 ilipokuwa”.

Soma na hizi

Tupia Comments