Top Stories

Polisi watibua ndoa ya Mwanafunzi “alitolewa mahari ng’ombe sita”

on

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watu wanne wakiwemo Wazazi kwa tuhuma za kumuozesha mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 12.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amesema baada ya kupata taarifa kuna ndoa ya mwanafunzi inafungwa walifika eneo la tukio wakiwa na maofisa maendeleo wa Halmashauri na kuwakamata watuhumiwa hao huku bwana harusi akitoroka.

“Ndoa ya mwanafunzi huyu wa darasa la tano ilikuwa inafungwa nyumbani kwao na aidha waliokamatwa ni Geni Bundala, Jumanne Shingimahi, Hawa Ramadhani na bwana harusi Khalifan Japhari(23) ambae bado jeshi hilo bado linamtafuta ili wachukuliwe hatua kali za kisheria,” RPC Magiligimba.

Kwa mujibu wa Kamanda Magiligimba, Mwanafunzi huyo aliolewa kwa mahari ya ng’ombe nane na fedha kiasi cha shilingi laki sita, sambamba na hilo mwanafunzi huyo amepelekwa kwenye kituo cha kulelea watoto waathirika wa mimba na ndoa za utotoni.

PROF. MKENDA AJIBU “SIJAUZA MLIMA KILIMANJARO WALA SIJAFUKUZWA KAZI”

Soma na hizi

Tupia Comments