Jeshi la Polisi Dar es salaam limewakamata Watuhumiwa wengine 167 wanaotuhumiwa kujihusisha na uhalifu wa kuvunja nyumba usiku, kujeruhi Watu kwa kutumia silaha za jadi kama mapanga, nondo na visu na kupora mali mbalimbali.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Nchini, Awadh Haji mbele ya Waandishi wa Habari leo amesema Watuhumiwa hao wamegawanyika katika makundi ambapo kuna wanaovunja na kupora na kundi linalopokea na kununua mali hizo za wizi.
“Tumekamata mali zilizoibwa maeneo mbalimbali ya Dar es salaam zikiwemo TV flat screen 23, Radio subwoofer mbili, computer desktop mbili na spika mbili za Subwoofer ambapo Watuhumiwa wamekutwa na mapanga 19, mikasi minne, jeki mbili na vifaa vya kuvunjia” amesema Kamishna Awadh Haji.