Habari za Mastaa

‘Ukiwa na njaa utafanya lolote hata kudanga nitadanga nipo serious’ Gigy Money

on

Muimbaji Gigy Money amewajibu watu waliokuwa wakimsema kuwa ameanza kufanya kazi kabla ya arobaini ya mtoto kitu ambacho siyo kawaida kama ilivyozoeleka, ambapo yeye kasema kuwa anafanya vile ili kumsaidia mwanae na atafanya lolote kwa ajili ya mtoto wake.

Gigy Money ambaye amewajibu watu hao kwa kuandika ujumbe wenye mafumbo kupitia Instagrama yake ameandika hivi…>>>“Ogopa sana mapenzi ya mama na mtoto yani Mama anaweza kujikuta anafanya lolote kwa ajili ya kesho ya mwanae ata awe chizi hawezi kumtupa mwanae haijalishi wakati wa mimba mangapi yamepita nachowaza saivi ni binti yangu tu ataaa kudanga ntadanga npo serious mjue nawale ambao mnanitukana kwann kipindi hiki nafanya kazi natoka kabla ya 40 Naomba”

“Niwajibu kiufupi kama mkubwa utaelewa kama mtoto endelea kunijazia comments za matusi yaaani ni iviii (utamaduni wa mtanzania ni njaaa ukiwa na njaaa unaweza fanya lolote sidhani kama ningekua napewa kila kitu ningetoka tu) so usilaumu kitabu tu kwasabu juu umeona fuvu ukajua iko kitabu kinahusu mazombie …. kisome kwanza. Ndio uogope Muwe na siku njema” – Gigy Money

Shilole ameingiza tani Moja ya Pilipili zake Sokoni, kafunguka Hapa

MWIJAKU “Mc Pilipili ameshindwa kumhudumia mtoto, kimaisha hawezi kunipata”

Soma na hizi

Tupia Comments