Top Stories

Rais Magufuli “kupinga Ushoga hadharani, Viongozi wachache wanaweza” (+video)

on

Rais Magufuli ameungana na Maaskofu, Mapadre, Watawa na Waumini wa Kanisa Katoliki kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Askofu Evaristo Chengula aliyefariki dunia November 21, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini DSM alikokuwa akipatiwa Matibabu.

 

Rais Magufuli amesema pamoja na majukumu yake ya kutoa huduma za kiroho Marehemu Askofu Chengula alisimamia ukweli ikiwemo kupinga hadharani ndoa na mapenzi ya jinsia moja licha ya kuwepo mashinikizo mbalimbali.

“Askofu Chengula alikua mkweli na alihubiri Injili kwa ukweli na hivi karibuni alizungumza kuhusu kupinga hadharani Ushoga, ni Watu wachache sana Viongozi ambao wanaweza kujitoa hadharani na kuzungumza ukweli uliopo kwenye Biblia takatifu” Rais Magufuli

 

AMBER RUTTY ANAO WADHAMINI WAWILI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

DAKIKA 240, SHOW YA ALIKIBA KAHAMA, NI BAADA YA MVUA KUBWA. BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

 

Soma na hizi

Tupia Comments