Michezo

Jurgen Klopp kataja mbadala wake ikitokea kaondoka Liverpool

on

Kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp katika mahojiano yake na Four Four Two amemtaja kocha ambaye anatamani awe mrithi wake katika kiti cha ukocha wa Liverpool ikitokea kaondoka timu hiyo.

Klopp anaamini kuwa kama ikitokea siku akaondoka Liverpool, mtu sahihi wa kurithi kiti chake ni nahodha wa zamani wa timu hiyo Steven Gerrard ambaya kwa sasa anaifundisha Rangers ya Scotland.

Gerrard akiwa Ranger kama timu yake ya kwanza kuanzia kazi aliisaidia kumaliza nagasi ya nne nyuma ya mabingwa Celtic kwa tofauti ya point 9, ila Gerrard ameiongoza timu hiyo katika michezo 76 ya mashindano yote na ameshinda 44 sawa na ushindi kwa asilimia 58.

Soma na hizi

Tupia Comments