Ajali

MAREKANI: Habari nyingine kuhusu Majeruhi watatu ajali ya Arusha

on

Tunakumbuka watoto watatu waliojeruhiwa kwenye ajali ya basi la Wanafunzi Karatu, Arusha wako Marekani katika Hospitali ya Mercy, Sioux City Iowa kwa matibabu ambapo mtoto wa mwisho kufanyiwa upasuaji ni Doreen aliyefanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye amekuwa mstari wa mbele kwenye harakati za kuwasaidia watoto hawa amesema tayari amekwenda Lucky Vicent kuchukua mitaala maana watoto hao wataendelea kufundishwa wakiwa Hospitali Marekani ambapo kuna Walimu wa Marekani waliojitolea watashirikiana na Walimu wa Tanzania.

Nyalandu ameziambia pia AyoTV na millardayo.com >>>  Madaktari wanasema itachukua miezi kadhaa na kwa uhakika wanasema Doreen atachukua zaidi ya miezi sita akiwa katika uangalizi wa karibu Hospitalini”

VIDEO: Historia ya eneo walikopata ajali Wanafunzi Arusha, itazame kwenye hii video hapa chini!!!

Soma na hizi

Tupia Comments