Kwa mujibu wa Kifungu cha 5. -(1) cha Sheria ya PPP, Sura 103, Kituo cha Ubia (PPP Centre) kimepewa jukumu la kutoa usaidizi wa kiufundi pamoja na mafunzo kwa Mamlaka za Serikali, zikiwemo Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs), katika kuibua, kuandaa, na kusimamia utekelezaji wa miradi ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP).