Ad
Ad

Michezo

Baada ya Pique wa Barcelona kuendelea na kauli zake za kejeli kwa Real Madrid, hizi ni kauli za Alvaro na Ronaldo …

on

Beki wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania Gerard Pique ameonekana kuwa na tabia kichokozi kwa wachezaji wa timu ya Real Madrid ya Hispania ambao ni wapinzani wa jadi wa klabu anayoichezea, Pique anatajwa kufanya ishara za kejeli kwa upande wa wachezaji wa klabu ya Real Madrid wakati ambao wanapata matokeo mabovu.

Pique anatajwa kuandika tweet katika mtandao, tweet ambayo moja kwa moja inaashiria kuwa alikuwa anafanya kejeli kwa timu ya Real Madrid, staa huyo wa FC Barcelona aliandika vikatuni vya emoji muda ambao Real Madrid wametangazwa kutolewa katika Kombe la Copa del Rey baada ya kumtumia mchezaji ambaye hakuwa na vigezo vya kucheza mechi dhidi ya Cadiz.

251020_heroa

Usiku wa December 8 baada ya Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 8-0 dhidi ya Malmoe FFAlvaro Arbeloa amefunguka kuhusiana ishu hiyo, “Pique anaonekana kutuchokoza ila itafika wakati sahihi tutamjibu” >>> Alvaro Arbeloa

Hii ni mara ya pili kwa Pique kumfanya kejeli kwa Real Madrid, baada ya mwishoni mwa msimu uliyopita kuongea kauli ya kejeli wakati wa sherehe za ubingwa za FC Barcelona ambapo Pique wakati wa kutoa maneno yake alimshukuru Kevin Roldan mwanamuziki wa Colombia ambaye alikuhudhuria Birthday Party ya Ronaldo saa chache baada ya Real Madrid kufungwa 4-0 dhidi ya Atletico,  ilitafsiriwa kama kamshukuru Kevin Roldan kwa kumpoza machungu Ronaldo.

Kwa upande wa Ronaldo hii ndio ilikuwa kauli yake “Vitu anavyo tweet Pique sidhani kama vinastahili comment yoyote kwani havina faida yoyote kwa jamii, siwezi kuvizungumzia kwa sababu kuzungumzia hivyo ni kupoteza muda” >>> Ronaldo

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments