AyoTV

VIDEO: ‘Tunapaza sauti ndugu zetu wanakufa lakini hakuna linalochukuliwa’-Profesa Jay

on

Naendelea kukusogezea Headlines za Bunge kila zinaponifikia, na leo May 25 2016 Bunge la 11 limeendelea kuijadili bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa siku ya pili mfululizo tangu ilivyoombwa jana na Waziri Jumanne Maghembe kiasi cha Sh. 135,797,787,000 .

Wabunge mbalimbali walipata nafasi ya kuchangia maoni yao, nakukutanisha na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu Profesa Jay aliposimama na kusema…>>>

Kama kweli tunataka tulinde rasilimali zetu na wanyama wetu tuwape wananchi elimu ili wajue vitu vya kufanya na vipi si vyakufanya, lakini sasa hivi ndugu zetu wanaokaa karibu na mbuga wameonekana kuwa wanateswa.

‘Na niwaambietu Mikumi kuna watu wengine tumezika nguo kwasababu hata maiti zao hatukuweza kuzipata kwasababu wamepigwa risasi ndani ya hifadhi. Kwa hiyo kutokana na hilo tunataka tuisisitize Serikali kama kweli mnataka tulinde rasilimali za Mikumi’

Tupunguze uadui huu kati ya Wananchi wanaoishi kwenye vijiji vinavyopakana kwenye hifadhi  na watu wa hifadhi. Tunapaza sauti ndugu zetu wanakufa lakini hakuna linalochukuliwa lolote

Full video ya Profesa Jay nimekuwekea hapa chini, ukimaliza kuitazama niachie maoni yako ili akipita baadae azisome

ULIIKOSA HII? WIZARA YA MALIASILI NA UTALII IMEOMBA KUPITISHIWA BILIONI 135 KAMA BAJETI YAKE IJAYO

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments