AyoTV

VIDEO: Bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa imetangazwa

on

March 1 2016 Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini (EWURA) ilitangaza bei mpya ya bidhaa za mafuta ya Petrol, Diesel na ya mafuta ya taa katika masoko yote ya jumla na rejareja ambapo bei hizo zitaanza kutumika kuanzia tarehe 2 march 2016.

Akiongea na waandishi wa habari Dar es salaam, Mkurugenzi wa huduma za nishati na maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema kuanzia tarehe 2 March bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la February 2016, kwa March 2016 bei ya rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa na 1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na 7.10% na mafuta ya taa yamepungua kwa Tsh 234 kwa lita sawa na 13.75%

kwa kiasi kikubwa , kupungua huku kwa bei za mafuta kwenye soko la ndani kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia

Unaweza kuitazama pia hii Video hapa chini wakati bei hizo zikitangazwa….

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments