Mix

Aliambiwa hatokuja kupata mtoto, miaka 60 baadae stori ni hiki kilichokutwa tumboni !!

on

ANCIANA DE 92 AÑOS PORTA FETO MOMIFICADO EN SU VIENTRELA BOCA 19 DE JUNIO 2015FOTOGRAFÍAS CHRISTIAN PAVEZ CISTERNA

Estela Melendez 91

Nimekutana na stori moja kutoka mji mdogo wa La Boca ulioko Chile ambako mwanamke wa miaka 91 amekutwa na mtoto tumboni ambapo mtoto ujauzito huo kaubeba kwa zaidi miaka 60.

Estela Melendez mwenye umri wa miaka 91 amekua akilalamika kwa zaidi ya miaka ishirini kwa kuwa na uvimbe mgumu tumboni mwake na hakuwahi kuhisi ana ujauzito na wala hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito.

ES2

Estela Melendez akiwa na baadhi ya ndugu zake

Baada ya madaktari kumfanyia vipimo na uchunguzi wa kutosha wamegundua ya kuwa mwanamke huyo alishika ujauzito akiwa na umri wa miaka 30 hivi, kitu ambacho kimewashangaza ndugu zake wengi ni kwamba yeye na mume wake waliambiwa hawawezi kupata watotoalafu leo zimekuja stori nyingine.

Estela Melendez amesema hakuwahi kuhisi dalili zozote kwa kipindi chote ila alijihisi uvimbe mdogo ukimuuma na kuacha kwa nyakati tofauti…alikuwa akipata maumivu mara mojamoja lakini zaidi ya hapo uvimbe huo umemkosesha raha kwa miaka mingi.

ES4

Hiki ndio kilichokutwa tumboni mwa Estela Melendez

Madaktari wamesema uvimbe huo hauna madhara yoyote kwa mwanamke huyo ila wanajianda kumfanyia upasuaji kuutoa uvimbe huo, kwa sasa Estela Melendez amelazwa hospitalini akisubiri kufanyiwa operation hiyo.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments