Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

#Exclusive: Dakika 5 za maamuzi mapya ya Prezzo kuhusu beef zake na Jaguar na Diamond on @AyoTV

on

Screen Shot 2014-05-13 at 3.33.40 AMKwa miaka na miezi baadhi ya makubwa yaliyoripotiwa na media hasahasa kwenye mtandao na radio ni kuhusu beef ya Prezzo na msanii mwezake Jaguar lakini pia beef nyingine ya hivi karibuni na Diamond Platnumz ambayo ilitokea mwaka 2013.

Prezzo aliwahi kunukuliwa akisema alikua hafahamu kama kuna msanii anaitwa Jaguar bali alijua ni aina ya gari ambapo Jaguar aliwahi kunukuliwa akimkosoa Prezzo kwa kutoa muziki wa kujisifia kila wakati.

Chanzo cha beef ya Diamond na Prezzo kinadaiwa kuwa maneno aliyoyatoa Diamond pale alipoalikwa kufanya show moja ya Matumaini akatoa maneno kwamba atamgaragaza Prezzo akiwa anamaanisha kwamba siku hiyo atafanya show nzuri kuliko Prezzo.

Ni mwanzo wa beef ambayo Prezzo amekiri ilitokana na kutoelewana tu na kwamba kiswili kilichotumiwa na Diamond sio kiswahili kilichozoeleka Kenya hivyo ilikua ngumu kwa Prezzo kuelewa ni lugha ya kibiashara na sio kwa ubaya.

@AyoTV na millardayo.com zimepata Exlusive ya Prezzo akizungumzia hizo beef na hawa wasanii wawili.

Unataka stori kama hizi zisikupite? kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi hivyo jiunge nami twitter kwa kubonyeza hapa HAPA pia instagram na facebook kwa kubonyeza INSTA >> FB

Tupia Comments