Waziri wa serikali ya awamu ya nne Prof. Mark Mwandosya ameingia katika list ya watu walionesha furaha yao baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kuachiliwa leo kutoka gerezani ambapo alihukumiwa kifungo cha miezi mitano.
Prof. Mwandosya ameandika katika ukurasa wake wa twitter >>> “Nikimpa hongera Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi kwa kuhitimu Chuo cha Uanasiasa, gereza la Ruanda, Mbeya. Kutofautiana vyama, itikadi na misimamo kusilete uhasama na uadui. Mungu Ibariki Tanzania.”
Kauli ya kwanza ya Sugu ‘Nilifungwa mwili ndani ya Magereza’