Rapper Jay Z alituma barua ya maombi kwa uongozi wa legend wa muziki Marekani marehemu Prince, na kuomba umiliki wa nyimbo zake ambazo mpaka kifo chake alikuwa hajazitoa. Inasemekana Jay Z alitenga dola za kimarekani milioni 40 kwa ajili ya kukamilisha deal hilo.
Baada ya kuzungumza na uongozi wa Prince umekataa kusaini deal hilo na rapper huyo, ukidai kuwa Jay Z alishawahi kuziachia albamu 15 za Prince kwenye mtandao wake wa Tidal miezi michache tu baada ya Prince kufariki bila kibali chochote, na wanaamini Jay Z aliingiza pesa ndefu hivyo kuna uwezekano wa kumfungulia rapper huyo kesi ya madai.
Hata hivyo inasemekana uongozi unaosimamia kazi za Prince unafahamu Jay Z alikubaliana na Prince kuwa atasimamia albamu yake ya “HitNRun Phase One” ya mwaka 2015 lakini hakuna nyaraka za mikataba zinazoonyesha malipo ya dolla 750,000 ambazo ndio zilipaswa kulipwa ili kufunga mkataba.
VIDEO: Kama ulimiss hii EXCLUSIVE: Nyumba ya milioni 700 wanayoijenga Navy Kenzo>>>
VIDEO: Gharama zilizotajwa kwenye malipo ya Nyumba aliyonunua Diamond Platnumz South Africa>>>