Top Stories

Maneno ya kwanza ya Profesa Jay baada ya kushinda kiti cha Ubunge. (+Audio)

on

Bado tupo kwenye headlines za uchaguzi 2015 ambapo msanii mkongwe wa HipHop Tanzania Joseph Haule (Profesa Jay) ni mmoja wa wawashindi wa kiti cha ubunge kwenye uchaguzi huu akiwa amechukua jimbo la Mikumi Morogoro na anachosubiri kwa sasa ni kuingia bungeni.

Prof. ameongea na millardayo.com >>>‘Nawashukuru sana wananchi wa Mikumi kwa kuniamini na kunipa dhamana hii kubwa, watanzania wameniamini kwa sababu ya upeo mkubwa ambao Mungu amenipa, naamini sana katika umoja na mshikamano….! na ndiomaana nimekuwa nasisitiza hata katika kampeni zangu, lazima tushikamane watu wote wa vyama vyote na hata wasio na vyama ili kuikomboa Mikumi yetu ‘ –

.

.

Changamoto kubwa ni maji, elimu, miundo mbinu pamoja na ajira, nitaendelea kuwatumikia wananchi wangu kwasababu wao ndio wamenituma Dodoma, mimi kuwa mwanamuziki halitonizuia kuwawakilisha wananchi…. nitaendelea kuwa mwanamuziki na huwenda nikafanya muziki ule wa juu zaidi kwasababu nategemea kukutana na watu wa juu zaidi’– PROFESSOR J

prof

Unaweza ukabonyeza play hapa chini kumsikiliza Professor Jay akizungumza kuhusu ushindi wake wa kiti cha Ubunge

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andikaAYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments