Matumizi makubwa ya fedha katika usajili ya klabu ya mabingwa wa Ufaransa Paris Saint Germain yameonekana kumtisha mwenyekiti wa mabingwa wa ulaya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge ambaye ameliambia shirikisho la soka UEFA kuchukua hatua dhidi ya klabu hiyo inayomilikiwa na matajiri wa Qatar, ikiwa wataonekana kwenye kinyume na sheria ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha.
Mwenyekiti huyo wa Bayern ametoa kauli hiyo akionyesha kutishwa na matumizi ya PSG na sasa amemwambia raisi wa UEFA Michel Platini kuiadhibu klabu hiyo ya Ufaransa ikiwa watakuwa wameenda kinyume na sheria ya Financial Fair Play.
“Ni vigumu kufikiria kwamba Paris Saint-Germain wanafuata sheria ya FFP. Wote tunajua wapi fedha zile zinapotoka, wametumia zaidi ya €200 million kwa msimu,” Rummenigge aliiambia SpoBiS convention.
“Matumaini yangu Michel Platini atafuatilia suala hili kwa umakini. Vilabu ambavyo havifuati sheria ya FFP itabidi vikumbane na adhabu. Ni wakati muafaka kwa UEFA. Vilabu vimekuwa na muda wa miaka mitatu kwenda sawa na vigezo vya FFP na UEFA inabidi isikubaliane na uvunjifu wowote wa sheria hii.
“Watu wanaweza wasikubaliane na Platini na mimi, lakini haitakiwa mtu mmoja tajiri kutoka Saudia Arabia au Russia atumie rasimali zake kutuamulia bingwa wa Champions leeague.”