Michezo

Makofi kwa PSG tafadhali…. Full Time yao vs Chelsea imewapa ushindi

on

Michezo ya marudiano hatua ya 16 bira ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea tena usiku wa March 9, kwa michezo miwili kupigwa barani Ulaya. Klabu ya Chelsea ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, wakati Zenit walicheza dhidi ya Benfica.

Kwa upande wa klabu ya Chelsea walikuwa Stamford Bridge chu kupambana na PSG ili waweze kusonga mbele hatua robo fainali kwa kuhangaika kutaka kuifunga klabu hiyo, ambayo mchezo wa kwanza, walifungwa 2-1 Paris Ufaransa.

2065

Hata hivyo jitihada za Chelsea ziligonga mwamba, baada ya PSG kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, hivyo Chelsea wametolewa kwa jumla ya magoli 4-2. Magoli ya PSG yalifungwa na Adrien Rabiot dakika ya 16 na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 67 na Chelsea kuambulia goli moja pekee lililofungwa na Diego Costa dakika ya 27.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments