social network

“Hakuna mtu mbaya” – Peter wa P-squire

By

on

P-squire ni moja kati ya makundi yanayoundwa na wasanii wenye heshima kubwa Africa na waliofanikiwa kuvuka boda kuutangaza muziki wa Africa duniani wakifanikiwa kutoa hit baada ya hit na kutunukiwa tuzo mbalimbali kubwa duniani.

Kwenye safari yao ya muziki, yapo mengi yaliyojitokeza ikiwa pamoja na kumpoteza mama yao mzazi mwaka 2012, kutengana kama kundi mwaka jana. Licha ya hayo yote P-squire linabaki kuwa kundi bora la muziki kutoka Africa

Peter ametumia ukurasa wake wa Instagram kupost picha yao ya zamani kuandika kuwa kipindi hicho walikuwa wanapambana kweli kweli #GameOver ambayo pia ni jina la Albam yao ya tatu,  akaandika pia #NobodyUgly akimaanisha hakuna mwenye sura mbaya. Kwa maana nyingine kuna tofauti kubwa baina ya wakati huo walipokuwa wanapambana na sasa ambapo pesa imekaa vizuri.

Video: Peter wa P Square kuhusu Diamond na Watanzania>>>

 

Soma na hizi

Tupia Comments