Habari za Mastaa

Unajua kitu kinachowapa hofu zaidi P Square? Majibu yao ni haya hapa..

on

 PSQURRR 2Peter na Paul Okoye kwa pamoja tunawajua kama P Square, ukubwa wa jina lao sio ndani ya Africa pekeyake… wana hits kibao ambazo zimewaweka kwenye ramaniya dunia pia.

Mafanikio yao yalianzia pale ambapo waliweka nguvu yao nyingi kwa kufanya muziki wakitumia lebo yao ya Square Records… December 2011 milango mingine mikubwa ikafunguka kwenye muziki wao, waliingia Mkataba kufanya kazi na lebo ya Akon Konvict Muzik.. kazi kama Beautiful Onyinye waliyomshirikisha Rick Ross na Chop My Money zilipenya sana nje ya Afrika, watu wakazidi kuwajua !!

Safari yao haikuwa rahisi, lakini unajua siri ya wao kuifungua milango yote ya mafanikio? Kuna kitu chochote wanachokihofia kwa sasa?

>>> “Siri ya mafanikio yetu ni kazi. Tunafanya sana kazi.. Juhudi zote tunazowekeza katika kazi yote ni hofu ya umaskini, tumeshaonja maisha ya umaskini mkubwa na tunaogopa sana umaskini, ndio maana utasikia tumewekeza hapa na kule yote ni kujikinga na umaskini.

Tumeshuhudia wasanii waliopata umaarufu na utajiri kabla yetu lakini leo hawana chochote cha kuonesha kwa juhudi zao, kitu hiki kinatuogopesha sana… Tuliwahi kuishi maisha ya kubanana baba, mama na watoto nane kwenye nyumba ya kupanga yenye vyumba viwili, chakula, ada, mavazi vilikuwa ni tatizo sana kwetu na kipindi hicho baba yetu alitusihi sana tuje kuwa viongozi wa maisha yetu wenyewe tusiopenda kufanya kazi chini ya mtu na ndio maana unawaona P Square wanafanya biashara zao wenyewe leo”.>>> Nukuu ya walichokisema P Square kwenye moja ya Interview.

MWIMBAJI BEN POL ALIVYONUSURIKA KIFO BAADA YA BOTI KUZAMA BAHARINI, TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments