Mix

Hii ni Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu mauaji na kisa kikiwa ni mapenzi.

By

on

polisiTaarifa kutoka Mtwara ambayo wana-amplify jeshi la polisi Mkoa wa mtwara ni kuhusu mauaji yaliyotokea huko Mtwara  ambayo chanzo chake kimeelezwa ni wivu wa kimapenzi uliokuwepo kati ya wapenzi hao.

Jeshi la Polisi limesema mauaji hayo yametokea Ligula B kata ya Ligula Tarafa ya Shangani mkoa wa Mtwara,ambayo yanamhusisha Habibu Dastan au Upson Milanzi[26] ambaye anatuhumiwa kumuua mpenzi wake Zuwena Mwapindi[27].

Kifo cha Zuwena kinasemekana ni baada ya kuchomwa na kisu kwenye ziwa  lake la upande wa kushoto,mtuhumiwa baada ya kufanya mauaji hayo alifanikiwa kutoroka lakini kwa ushirikiano wa wananchi na jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa eneo la Namayakata Tarafa ya Ziwani,Kata ya Nanguluwe,Wilaya ya Mtwara vijijini.

Mtuhumiwa anategemewa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika,millardayo.com imepata picha za marehemu lakini kutokana na sababu za kimaadili hatutoweza kuziweka hii chini ni picha ya mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.

mtuhumiwa

 

Tupia Comments