Mix

Pale ambapo mbwa anaamua kutembelea mgonjwa Hospitali…(Video)

on

dogKwa nchi za wenzetu mbwa ni sehemu ya familia, huduma anayopewa ni sawa tu na binadamu yoyote ambaye anaishi kwenye nyumba husika.

Hii inaweza kukushangaza kiasi fulani kutoka Marekani, mbwa ambaye jina lake ni Sissy aliona muda unakwenda hamuoni mlezi wake, akaamua kwenda hadi hospitali alikokuwa amelazwa mlezi wake huyo.

Nancy Frank ambaye ndiye aliyemfuga mbwa huyo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mercy Medical Center akitibiwa cancer kwa muda wa wiki mbili huku mbwa wake akiwa amemuacha nyumbani kwake, kilichomshtua ni kitendo cha mbwa huyo kumfuata mpaka hospitali.

Mbwa alifika Hospitali akiwa na maelezo kwenye shingo, walinzi walimtambua na kumpeleka kwenye chumba alichokuwa amelazwa Nancy.

Mara nyingi wanyama kama mbwa na paka wana uwezo wa kurudi nyumbani wanakofugwa hata kama wakipelekwa mbali, lakini hii ya mbwa kumtafuta anayemfuga hospitali alikolazwa ni kitu kilichoshangaza wengi.

Unaweza kucheki video ya story hiyo hapa.

https://www.youtube.com/watch?v=lMawnI5m-tE#t=10

Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments