Rais Vladimir Putin wa Russia ameamuru mwongozo wa utumiaji silaha za nyuklia wa nchi hiyo ufanyiwe mabadiliko akionya pia kuwa nchi yake inaweza kujibu mapigo kwa silaha za nyuklia ikiwa itashambuliwa kwa silaha za kawaida zilizotolewa na dola linalomiliki silaha hizo.
Akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama la Russia uliorushwa hewani na televisheni ya nchi hiyo, Putin amebainisha kuwa kulingana na marekebisho na mabadiliko yaliyopangwa kufanyika, shambulio dhidi ya nchi hiyo na nchi isiyo na silaha za nyuklia kwa “kushiriki au kuunga mkono dola la nyuklia” litaonekana kama “shambulio la pamoja dhidi ya Shirikisho la Russia”.
Katika hotuba yake hiyo, Putin hakufafanua ni lini mabadiliko ya Mwongozo wa nyuklia wa Russia yataanza kutumika.
Hata hivyo, katika miezi ya karibuni, maafisa waandamizi, akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Ryabkov na Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov wamekuwa wakijadili mabadiliko yanayoweza kutokea katika mwongozo huo. Mwishoni mwa Agosti, Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov alisema hati hiyo “inafanyiwa mapitio.