Rais wa Urusi Vladmir Putin ameipa mbuga kuu ya wanyama ya Korea Kaskazini zaidi ya wanyama 70 akiwemo simba mmoja na dubu wawili katika onyesho jingine la uhusiano unaoimarika kati ya Moscow na Pyongyang.
Waziri wa mazingira wa Putin, Alexander Kozlov, aliwapeleka wanyama hao katika mji mkuu wa Korea Kaskazini wakiwa ndani ya ndege ya mizigo, ofisi ya Kozlov ilisema kwenye akaunti yake rasmi ya Telegram siku ya Jumatano.
Wanyama hao kutoka Moscow pia walijumuisha ng’ombe wawili, kasuku watano na dazeni ya ndege aina ya kwale pamoja na bata, ofisi ya Kozlov ilisema.
Zawadi hiyo inakuja wiki kadhaa baada ya Marekani na Korea Kusini kufichua kuwa Korea Kaskazini imetuma maelfu ya wanajeshi kupigana pamoja na Urusi nchini Ukraine.