Puto zenye uzito wa taka zilizotumwa na Korea Kaskazini ziligonga majengo ya ikulu ya rais wa Korea Kusini siku ya Jumatano, maafisa wa usalama ambao wamehamasisha timu za kukabiliana na kemikali wameliambia shirika la habari la AFP.
Hii ni mara ya kwanza kwa ikulu ya rais wa Korea Kusini, iliyoko katikati mwa mji wa Seoul na kulindwa na makumi ya askari na eneo lisilo na ndege, kupigwa moja kwa moja na maelfu ya puto za taka zilizozinduliwa na Pyongyang tangu mwezi Mei kama sehemu ya vita vya propaganda kati ya nchi hizo mbili.
“Kikosi cha kukabiliana na vita vya kemikali, kibayolojia na radiolojia kimepata puto za takataka kwa usalama,” huduma ya usalama ya rais imeliambia shirika la habari la AFP.
“Baada ya uchunguzi, matokeo yamethibitisha kwamba hakukuwa na hatari au uchafuzi wa kitu,” imeongeza. Makao makuu ya jeshi la Korea Kusini lilionya kuhusu kurushwa kwa puto nyingine kutoka Korea Kaskazini na mamlaka ya Seoul ilitoa tahadhari siku ya Jumatano asubuhi.
“Mkipata puto zimeanguka chini, lsiziguse na mripoti kwa kitengo cha kijeshi kilicho karibu au kituo cha polisi,” walionya.