Maajabu

Kuna hii hukumu aliyopewa jamaa kwa kosa la kula nyama ya chatu !!

on

Python

Moja ya aina ya story zinazovutia watu wengi ni pamoja na story ambazo zina matukio ya ajabu ama matukio ambayo yako tofauti na watu walivyozoea.

Kutoka Zimbabwe kulikuwa na story ambayo ilikaa kwenye headlines sio za Zimbabwe tu, ila duniani kote; ishu ya Rais wa nchi hiyo kuanguka wakati akishuka ngazi.

Leo nakupa hii nyingine ya jamaa ambaye amejikuta akiangukia kwenye mikono ya hakimu wa Mahakama na kuhukumiwa kifungo cha miaka tisa jela kwa kosa la kula nyama ya chatu !.

Jamaa huyo, Archwell Maramba alijitetea kwamba mara nyingi amekuwa akila nyama hiyo ili kutibu maradhi ya uti wa mgongo na imekuwa ikimsaidia kwa kiasi kikubwa sana, utetezi ambao Mahakama haikuonekana kuujali.

Katika upelelezi wa Polisi walikuta ngozi ya chatu iliyokaushwa pamoja na nyama ndan ya nyumba ya Maramba.

Hukumu hiyo imetokana na jamaa huyo kuonekana akikiuka sheria ya uhifadhi wa chatu, ambao ni sehemu ya viumbe ambavyo vinatakiwa kuhifadhiwa na kulindwa.

Nitaendelea kukusogezea kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments