Habari za Mastaa

Soudy Brown kawapata Q Chillah na TID baada ya kudaiwa kutaka kupigana Club

on

Kupitia Uheard ya XXL ya Clouds FM leo July 25, 2017 mtangazaji Soudy Brown ameipata na kutusogezea hii story inayowahusu mastaa wakongwe wa Bongofleva Q Chillah na TID kutaka kupigana wakiwa Club.

Soudy Brown amewatafuta wote wawili ambapo kila mmoja amezungumza kwa upande wake huku TID akisema alishindwa kuvumilia utani wa Q Chillah.

>>>”Hamna kilichonuka kwani yeye amekuambiaje? Hamna tatizo lolote, hamna kitu chochote kibaya. Siyo kawaida yetu kutoleana mapovu halafu unajua sisi ni watu wazima sasa, hivi vitu vyetu tunaweza kuvirekebisha wenyewe. Tumekutana tu bahati mbaya sehemu ya starehe. Hakuna mambo ya mademu, sijawahi kushare mwanamke na mzee Mnyama hata mara moja.” – Q Chilah.

“Siyo mimi labda unawasikiliza watu wengine. Ilikuwa hivyo hivyo tu mimi nilikuwa nimekaa zangu Q Chillah akawa anapiga story zake anaweka na utani lakini kulikuwa hakuna ugonvi. Utani wake muda mwingine unakuwa mzito sana, anaongea sana mimi nitafanyaje nikimchukia anakuja tena kesho” – TID.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full Story...

 

VIDEO: Baraka kaondoka Rockstar4000…kaeleza mipango yake 

Soma na hizi

Tupia Comments