Ad

Mix

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo baada ya uteuzi wa Dr Mwakyembe na Prof. Palamagamba

on

Asubuhi ya March 23 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli alifanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri kwa kumteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dr Harrison Mwakyembe kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Huku akimteua Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, baada ya uteuzi huo Rais Magufuli jioni ya leo March 23 2017 amefanya uteuzi mwingine tena kwa mteua Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu Ikulu.

Kabla ya uteuzi huo wa Rais Magufuli aliyoufanya leo, Alphayo Kidata alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini nafasi hiyo ipo wazi na itazibwa baadae, Alphayo Kidata anarithi nafasi ya Peter Ilomo ambaye amestaafu.

VIDEO: Maamuzi ya JPM baada ya kufanya ziara ya kushitukiza bandari DSM

Soma na hizi

Tupia Comments