Michezo

Kutoka makao makuu ya CAF, hii ni habari kubwa kwa Serengeti Boys leo

on

Shirikisho la soka barani Afrika CAF lenye makao makuu yake Cairo Misri, leo February 3 2017 kupitia kwa shirikisho la soka Tanzania TFF limeipitisha timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) kupata nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana (AFCON-U17).

CAF wametoa taarifa hizo baada ya Tanzania kushinda rufaa yao waliyoikata dhidi ya timu ya Congo Brazzaville ambao walichezesha mchezaji aliyezidi umri wakati wa mchezo dhidi ya Serengeti Boys, hivyo Serengeti Boys wanapewa nafasi hiyo baada ya Congo kushindwa kumpeleka mchezaji wao aliyedaiwa kuzidi umri kufanyiwa uhakiki wa umri wake.

Langa Lesse Bercy anayedaiwa kuzidi umri pichani kulia

Kama utakuwa unakumbuka vizuri shirikisho la soka Tanzania TFF lilikata rufaa kwa CAF kupinga Congo kumchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy aliyedaiwa kuvuka umri wa miaka 17, hivyo alicheza mchezo dhidi ya Serengeti Boys kimakosa.

Tweet ya Waziri wa michezo Nape Nnauye

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments