AyoTV

VIDEO: Simba na Yanga wamekataa kucheza na Mabingwa wa Afrika, vipi Azam FC?

on

Siku moja imepita toka mabingwa wa Afrika Mamelod Sundows ya Afrika Kusini wawasili Tanzania kwa ajili ya michezo ya kirafiki na maandalizi ya msimu mpya, Mamelod wamekuja na kutaka kucheza na Simba na Yanga lakini vilabu hivyo vimekataa ndio jana wameomba kucheza na Azam FC.

Simba na Yanga wamekataa kwa kigezo kuwa hawawezi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mamelod wakiwa wapo katikati ya Ligi, kwa upande wa Azam FC wao vipi afisa habari wao Jafari Iddi ameongea leo na waandishi wa habari.
“Mamelod wamekuja Tanzania kwa ajili ya maandalizi yao ya msimu na wameomba kucheza na Simba, Yanga na Azam FC lakini Azam FC tumepokea mualiko jana na tumekubali kucheza nao licha ya kuwa tuna mchezo mgumu Jumamosi dhidi ya Ndanda FC lengo ni kujenga mahusiano mazuri”

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments