Habari za Mastaa

PICHA: Neymar kwenye penzi jipya na staa wa Pop?

on

Msanii wa muziki wa Pop Anitta ameanza kuingia katika tuhuma za kudaiwa kutoka kimapenzi na mwanasoka wa Brazil ambaye pia ni mchezaji wa Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa Neymar, Anitta ameanza kuhusishwa kuwa katika mahusiano na Neymar baada ya ukaribu kuzidi.

Anitta na Neymar wameonekana wakiwa beneti katika jiji la Rio De Janeiro nchini Brazil, ukaribu ambao umeanza kuzua utata mitandaoni kuwa inawezekana wawili hao kuna kitu kinaendelea, Anitta ni moja kati ya wasanii wa Pop maarufu nchini Brazil na Amerika ya Kusini na amekuwa akifanya kazi zake kwa kutumia lugha ya kireno.

Neymar na Anitta wakiwa Rio De Janeiro katika tamasha la Sambadrone wameonekana wakikumbatiana na ku-kiss kitu ambacho kinaaminika kuwa kuna uwezekano wawili hao wakawa mapenzini, Neymar alithibitika kuachana na girlfriend wake ambaye ni muigizaji maarufu nchini Brazil Bruna Marquezine toka October 2018.

VIDEO: MILLARDAYO, IMENITOA MACHOZI, BOSS RUGE AMENIIBUA NAJIULIZA NANI ATATUSHIKA MKONO

Soma na hizi

Tupia Comments