Top Stories

Askari nane waliotaka rushwa ya Bilioni 1, Watorosha dhahabu wafikisha Mahakamani (+video)

on

Watuhumiwa 12 wakiwemo Polisi Wanane wanaotuhumiwa kuhusika na sakata la kusafirishwa kwa dhahabu iliyokamatwa Kilo 323.6 wamefikishwa Mahakamani na kusomewa jumla ya mashtaka 12 ikiwemo Kuhujumu Uchumi na Kutakatisha fedha.

Miongoni mwa Watuhumiwa hao  ni pamoja na Polisi nane wanaodaiwa kuhusika katika utoroshaji wa dhahabu zaidi ya  Kilogramu 300 pamoja na Wafanyabiashara Sajid Hassan na Hassan Hassan wenye asili ya kiasia pamoja na Kisabo Kija Mkinda na Emanuel Ntemi.

Mbele ya Hakimu mkazi, Gwai Sumai , Wanasheria watatu wa Serikali, Castus Ndamgoba, Robert Kidando na Jacline Nyantori, Watuhumiwa hao wanasomewa mashtaka 12 yanayohusu Uhumujumu uchumi, kuomba na kupokea rushwa sanjari na kutakatisha fedha.

RC MWANRI AWAIBUKIA WALIOFUNGA NDOA NA MWANAFUNZI “MNOKO CHIKICHII NIMEWASUKUMIA NDANI”

Soma na hizi

Tupia Comments