Siku 13 baada ya uongozi wa Azam FC kutangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu na benchi lake la ufundi kutokea Hispania Zeben Hernandez, leo January 10 2017 wamemtangaza kocha mpya anayekuja kurithi nafasi ya Zeben.
Azam FC imetangaza kuingia mkataba wa miezi sita wenye kipengele cha kuongezewa mkataba zaidi na kocha Aristica Cioaba raia wa Romania mwenye umri wa miaka 45, Cioaba ameingia mkataba na Azam FC leo visiwani Zanzibar na yupo uwanjani kushuhudi mchezo wa nusu fainali wa Azam FC dhidi ya Taifa Jang’ombe.
Kama humfahamu vizuri Aristica Cioaba amewahi kuvifundisha vilabu kadhaa vya soka barani Afrika kama kuwa kocha msaidizi wa Raja Casablanca ya Morocco 2005, Al-Masry ya Misri 2006 lakini kabla ya kujiunga na Azam FC alikuwa kocha mkuu wa Aduana Stars ya Ghana.
Cioaba pia ana sifa ya kutodumu na klabu moja kwa muda mrefu kwa mujibu wa Wikipedia Cioba kuanzia mwaka 2005 hadi 2016 ni FC Bals pekee ndio aliyodumu nayo kwa miaka miwili nyingine zote ni chini ya miaka miwili.
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4