Nahodha wa timu ya taifa ya Togo Emmanuel Adebayor ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga na timu kadhaa, leo January 31 tukiwa tunaelekea kufunga dirisha la usajili, ametangazwa kusajiliwa na timu ya Istanbul Basaksehir na atakuwa akivaa jezi namba 26.
Adebayor amejiunga na timu ya Istanbul Basaksehir ya Ligi Kuu Uturuki kwa mkataba wa miezi 18, Adebayor ambaye alikuwa hana klabu toka aachane na Crystal Palace mwishoni mwa mwaka jana, alikuwa Uturuki kwa ajili ya kufanya mazunguzo na Besiktas lakini walishindwana mshahara na vinara hao wa Ligi.
Emmanuel Adebayor alikuwa anataka Besiktas wamlipe mshahara wa pound milioni 3 wakati wao walikuwa wanataka wamlipe pound milioni 2, hivyo akaamua kuachana nao na kujiunga na Istanbul Basaksehir waliyopo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Uturuki inayoshirikisha timu 18.
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4