Michezo

VIDEO: Interview ya Samatta baada ya kuifungia Genk katika ushindi wa 1-0 vs AS Eupen

on

Usiku wa January 21 2017 nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji, aliiwezesha timu yake kupata ushindi wa goli 1-0 ugenini katika mchezo dhidi ya wenyeji wao AS Eupen.

Goli la Samatta alifunga dakika ya 82 kwa kichwa baada ya kutumia vyema kona safi iliyopigwa na Ruslan Malinovskiy na kuifanya KRC Genk kuondoka na point tatu ugenini, baada ya mchezo huo Samatta alifanya interview na kueleza mambo kadhaa ikiwemo kutofunga kwa muda.

“Ni kweli ni muda mrefu kidogo nilikuwa sijafunga na nilikuwa nahitaji kufunga ili nipate kujiamini zaidi, nafikiri mchezo ujao nitakuwa najiamini zaidi kuliko nilivyokuwa sijafunga, kukaa bila kufunga kwa muda wakati mwingine inatokea mimi ni binadamu”

“Kuna wakati nafanya vizuri nafunga magoli mazoezini lakini ukija katika mechi inakuwa tofauti, sielewi kwa nini, lakini huwa nazidi tu kuongeza jitihada na kuomba Mungu tu, kuhusu kumaliza katika nafasi za kucheza michuano ya kimataifa huwezi kusema haiwezakini hadi Ligi imalizike”

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments