AyoTV

VIDEO: Baada ya kuachana na Taifa Stars, Yanga wametangaza kumpa kazi mpya Mkwasa

on

January 31 2017 uongozi wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans kupitia makamu mwenyekiti wake Clement Sanga wametangaza rasmi na kumtambulisha aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa kuwa katibu wao mkuu mpya.

Yanga wamempa kazi ya ukatibu mkuu Mkwasa nafasi ambayo ilikuwa inakaimiwa na Baraka Deusdedit toka aondoke Dk Tiboroha aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo, Baraka sasa anarudi katika nafasi yake ya mwanzo ya idara ya fedha na Mkwasa ndio katibu mkuu wao mpya.

Boniface Mkwasa

“Taratibu za kumpata katibu mkuu zimekamilika Baraka alikuwa anakaimu hakuwa amethibitishwa kuwa katibu mkuu, taratibu zimefanyika na kujiridhisha kuwa Boniface hakuwa pekeake lakini yeye ndio amepita kuwa katibu mkuu wetu mpya” >>>Clement Sanga

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments