Michezo

Wakongwe wa Man U hawajafurahishwa na Pogba na Lingard kucheza wimbo wa Wizkid

on

Headlines za mastaa wa timu ya Manchester United Paul Pogba na Jesse Lingard kurekodiwa video wakicheza wimbo wa Wizkid na Drake na kisha Pogba kuipost instagram, inazidi kuleta maoni na maneno ikiwa ni saa kadhaa kabla ya Man United kulazimishwe sare tasa na Hull City.

Pogba na Lingard

Pogba na Lingard ambao wamekuwa na utamaduni wa kushangilia magoli yao kwa kucheza muziki, wamekuwa wakijadiliwa sana wiki hii kufuatia kupenda kuishi maisha ya kupost video instagram huku Man United ikiwa haifanyi vizuri na sasa mchezaji wa zamani wa Man United Paul Ince ameongea.

Paul Ince

“Mimi na Ryan Giggs tulikuwa tunapenda kushangilia magoli kwa kucheza enzi zetu na tulikuwa  tunaweka katika mitandao ya kijamii kama tumejisikia kufanya hivyo…… lakini unafanya hivyo ukiwa nafasi ya 5 au ya 6 katika Ligi ??? enzi ya Bryan Robson, Peter Schmeichel na Mark Hughes wangeweza kutuchinja kama tungefanya hivyo halafu tupo nafasi ya 5 au 6, huo sio msingi wa Man United, unatakiwa kushinda ndio unasherehekea” >>> Paul Ince

Licha ya baadhi ya mashabiki na Wachambuzi wa soka kuwakosoa Pogba na Lingard, Paul Ince sio staa wa kwanza wa zamani wa Man United kuonesha hisia zake wiki hii za kutopenda tabia ya Pogba na Lingard kupost instagram wakati timu yao haifanyi vizuri na ipo nafasi ya 6 katika msimamo wa EPL.

Rio Ferdinand

“Kama ningekuwa Man United kwa sasa nisingefurahishwa na hili hata kidogo, wanatakiwa wajue kuna muda na mahali huu sio wakati sahihi wa wao kufurahia, mimi ni mtu wa kupenda kufurahi lakini nahisi Pogba anaonekana ana furaha tu na hali ya sasa ya Man United”>>> Rio Ferdinand


VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments