Michezo

VIDEO: Kwa mara ya pili mfululizo Samatta anaifungia KRC Genk katika ushindi wa 3-0

on

Ni siku kadhaa zimepita toka mtanzania Mbwana Samatta aifungie  goli peke lililoipa point tatu timu yake ya KRC Genk dhidi ya AS Eupen na baada ya hapo kufanya mahojiano na kuahidi kuwa mchezo ujao atacheza kwa kujiamini zaidi kutokana na kufunga goli hilo.

Kauli yake imedhihirika usiku wa January 24 2017 katika mchezo wake wa pili toka acheze mchezo wake wa kwanza na kutoa kauli hiyo, Samatta katika mchezo wao wa pili ambao KRC Genk ilicheza dhidi ya Kortrijk katika uwanja wao wa Luminus Arena na kupata ushindi wa 3-0.


Katika ushindi wa goli 3-0 mtanzania Mbwana Samatta ameendelea kuwa hodari wa upigaji vichwa, kutokana na kutumia vyema krosi iliyopigwa na  Schrijvers dakika ya 42 na kufunga goli la pili kwa KRC Genk, goli hilo linakuja ikiwa ni dakika 38 zimepita toka Siebe Schrijvers aifungie Genk goli la kwanza na Alejandro Pozuelo akafunga goli la tatu dakika ya 68.


VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments