AyoTV

AUDIO: Maamuzi ya waziri Nape baada ya kuona uharibifu wa viti Taifa

on

October 2 2016 siku moja baada ya kuchezwa kwa mchezo wa kihistoria kati ya Simba na Yanga uwanja wa Taifa Dar es Salaam, waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye alitembelea uwanja wa Taifa kujionea uharibifu wa viti uliotokana na mashabiki wakati wa mchezo wa Simba na Yanga, Nape ametembelea na kuamua kuzifungia Simba na Yanga kutumia uwanja huo.

“Bahati mbaya sana mechi ya jana ilikuwa nzuri lakini ikaharibiwa na watu ambao sio wastaarabu walioamua kuharibu miundombinu ya uwanja wetu wa Taifa, Simba walipofungwa wakang’oa viti, ni kweli tutakamata mgao wao wa mapato kufidia uharibifu lakini uwanja huu hautatumika tena na timu za Simba na Yanga hadi tutakapoamua vinginevyo”

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments