Alhamisi ya January 19 2017 staa wa soka wa kimataifa wa Argentina aliyewahi kuchezea timu za West Ham United, Man United na Juventus Carlos Tevez amewasili China baada ya siku kadhaa nyuma kusaini mkataba wa kujiunga na timu ya Shanghai.
Tevez anawasili kujiunga na timu hiyo akiwa kavunja rekodi ya kulipwa mshahara ya Lionel Messi wa FC Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambao ndio walikuwa wachezaji wanaoongoza kulipwa mshahara mkubwa zaidi duniani kabla ya Oscar na Tevez kujiunga na Shaghai.
Hivyo kwa sasa Tevez ndio atakuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani akifuatiwa na Oscar aliyejiunga na Shaghai pia akitokea Chelsea, kwa wiki Tevez atakuwa akilipwa mshahara wa pound 615000 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 1.6 za kitanzania.
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4