Michezo

CONFIRMED: Aliyekuwa katibu mkuu wa Simba Patrick Kahemele ameacha kazi

on

Usiku wa January 24 2017 zilianza kuenea habari katika mitando ya kijamii kuhusiana na aliyekuwa katibu mkuu wa Simba Patrick Kahemele kuacha kazi ya ukatibu mkuu wa timu hiyo, sababu ikitajwa kuwa ni kuamua kurudi Azam TV.

Patrick Kahemele ambaye alikuwa katibu mkuu wa Simba ameacha kazi na kujiunga na Azam TV na sasa atarithi nafasi ya Charles Hilary ya kuwa Director of Sports Azam TV na Charles Hilary amebadilishiwa majukumu na kuwa Director of Television Productions.

Kahemele ambaye amewahi kufanya kazi na Azam FC ameamua kurudi na kujiunga na kampuni ya Azam TV ambayo pia aliwahi kufanya nayo kazi, kama utakuwa unakumbuka vizuri ni miaka miwili na nusu imepita toka Kahemele aache kazi Azam TV na kuendelea na majukumu yake mengine.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments