Michezo

PICHA: Yanga wameshindwa kupata ushindi dhidi ya Zanaco FC, Club Bingwa Afrika

on

Mchezo wa kwanza wa round ya pili ya michuano ya Club Bingwa Afrika kati ya Dar es Salaam Young Africans dhidi ya Zanaco FC ya Zambia ulichezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga waliingia kucheza mchezo wao wa pili baada ya kuitoa N’gaya Club ya Comoro.
 Zanaco FC walifuzu kucheza round ya pili baada ya kuwatoa Mabingwa wa Rwanda APR. Kwa mujibu wa ratiba Yanga wameanza kucheza nyumbani dhidi ya Zanaco na kukutana na upinzani mkubwa licha ya kocha wao George Lwandamina kuifahamu Zanaco kutokana na kuifundisha soka Zambia kwa muda mrefu.
Uzoefu wa Lwandamina kufahamu soka la kwao Zambia haijaisaidia Yanga na kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana goli 1-1, Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 38 kupitia kwa  Simon Msuva lakini Zanaco walisawazisha goli hilo dakika ya 78 kupitia kwa Attram Kwame.
Yanga sasa watalazimika kuhakikisha wanapata ushindi ugenini March 18 watakaporudiana na Zanaco nchini Zambia au sare ya kuanzia magoli mawili kwa mawili ili wafuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Club Bingwa Afrika.

VIDEO: ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1

Soma na hizi

Tupia Comments